ELIMU NA UMUHIMU WA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI TANZANIA KWA MAENDELEO YA NCHI

Unaposikia neno “USHIRIKA” wengi wetu tunapata picha kwamba ni swala linalowahusu wakulima na ni kwa baadhi ya maeneo fulani tu! Dhana hii si kweli hata kidogo. Ushirika ni mfumo unaowaunganisha jamii fulani kwa hiari yao wenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote ili wawezekuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kutatua changamoto zinazo wakabili kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mh. raisi, najua unajua umuhimu wa vyama vya ushirika vile vyama vya msingi, vyama vikuu na vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa (saccos). Vyama vya ushirika ni kiunganishi tosha kati ya serikali na wakulima, vikitumika ipasavyo ni rahisi serikali kuwafikia wakulima moja kwa moja na hivyo kuwa rahisi kwa serikali kusimamia miradi yake kwa wananchi. Lakini pia vyama vya ushirika moja ya kazi zake ni kutafuta masoko ya vinavyo zalishwa na wanachama wake, ni vigumu sana kwa mkulima peke yake kupata soko la uhakika kulinganisha  na akiwa kwenye chama cha ushirika. Mkulima peke yake ni ngumu sana kushindana sokoni kutokana na uhalisia wa dunia ya leo yenye teknolojia inayokua kila kukicha. Kuna vyama vya ushirika mazoa vya kahawa, pamba, mkonge tuliona jinsi vilivyo kuwa na nguvu kiuchumi, vyama kama kama Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU), Nyanza Cooperative Union (1984) Limited (NCU), Coastal Region Cooperative Union (CORECU), Morogoro Region Cooperative Union n.k, lakini pia tunaweza kuanzisha vyama vya ushirika kwa wakulima wa miwa kwenye viwanda vya sukari, wakulima wa mpunga, wakulima wa korosho, wakulima wa mbaazi, wakulima wa vitunguu, wakulima wa nyanya, wakulima wa maharage, dengu, wafugaji n.k

Mh.raisi, faida za kuwa na vyama imara vya ushirika ni nyingi zikiwemo zifuatazo;

  1. Fursa za ajira. Vyama vya ushirika ni chanzo kikubwa cha uhakika cha kutoa ajira, kuna maafisa ushirika wilaya, mkoa, kanda, wasimamizi wa vyama vya ushirika, mameneja wa vyama vya ushirika, wahasibu wa vyama vya ushirika, washauri wa vyama vya ushirika, maafisa mipango wa vyama vya ushirika n.k

Chuo cha ushirika kinazalisha wataalamu wengi sana katika fani ya usimamizi wa vyama vya ushirika kila mwaka lakini matunda yake hayatumiki ipasavyo sababu hakuna pa kuwapeleka na mwisho wa siku itaonekana kozi zinazohusu ushirika hazina tija teja nchini Tanzania wakati sio kweli, Tanzania tunahitaji ushirika kwa kiasi kikubwa sana kutokana na mazingira yetu yalivyo. Watu wanapo zungumzia ushirika wanajua moja kwa moja ni kilimo tu! Dhana hii sio kweli kabisa, ushirika upo kwenye kila nyanja, miaka ya karibuni kumekuwepo na wajasiriamali wengi sana wadogo ambao kwa mmoja mmoja imekuwa ngumu kufikia soko la kikanda lakini kupitia ushirika tungeweza kufikia soko hilo kwa urahisi zaidi. Wajasiriamali wanatengeneza sabuni za miche, sabuni za maji, madawa ya kusafishi vyoo, pilipili, penunt butter, viungo vya chai, nguo, viatu, wanafuga kuku wa mayai na kuku wanyama n.k Kama wasomi kwenye fani ya ushirika tungepewa nafasi ya kuwafikia na kufundisha elimu hii kwenye jamii basi si ajabu leo hii tungekuwa tuna vyama vya ushirika vya watengeneza nguo, vyama vya ushirika vya wategeneza viatu, vyama vya ushirika vya wasindikaji wa vyakula, vyama vya ushirika vya wafuga kuku n.k

No comments:

Post a Comment

BENKI KUU YA USHIRIKA TANZANIA ''TANZANIA COOPERATIVE BANK......''

 Benki kuu ya Ushirika nchini Tanzania yenye makao yake makuu jijini Dodoma! inatazamiwa kuwa ni mkombozi wa vyama vya Ushirika nchini, Je, ...